logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uhuru,Raila na Ruto wawasili katika ukumbi wa Bomas katika hafla ya uzinduzi wa BBI

Ruto aliwasili katika ukumbi huo saa 10:30 baada ya kinara Raila Odinga kuwasili.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri26 October 2020 - 08:30

Muhtasari


  • William Ruto awasili katika ukumbi wa Bomas kuhudhuria uzinduzi rasmi wa BBI
  • Uhuru alilakiwa na kukaribishwa na naibu wa William Ruto kinara wa ODM Rial Odinga, spika Ken Lusaka na waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i

Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika ukumbi wa Bomas dakika chache kabla ya saa tano asubuhi.

Uhuru alilakiwa na naibu wake William Ruto, kinara wa ODM Rial Odinga, spika Ken Lusaka na waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i.

Ruto aliwasili katika ukumbi huo saa 10:30 baada ya kinara Raila Odinga kuwasili.

Wakenya wengi walikuwa njia panda endapo Ruto angelihudhuria hafla hiyo kutokana na msimamo wake dhidi ya ripoti hiyo.

Wakati Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Upinzani Raila Odinga walikabidhiwa rasmi ripoti hiyo katika Kisii State Lounge, Ruto alisusia hafla hiyo na kuhudhuria mazishi katika kaunti ya Uasin Gishu ambapo alikosoa ripoti hiyo.

Viongozi wa humu nchini wengi wamehudhuria hafla hiyo huku rais akitarajiwa kuongoza zaidi ya wakenya 6,000 walioalikwa kuhudhuria uzinduzi rasmi wa ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI).


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved