Naibu rais William Ruto anatarajiwa katika ukumbi wa Bomas hii leo katika uzinduzi wa BBI ili kumkaribisha rais Uhuru Kenyatta, hii ni baada ya kususia kuhudhuria mkutano wa ripoti ya BBI wiki jana.
Badala yake Ruto alihudhuria mazishi ya mwakilishi wadi wa Huruma aliyeaga dunia kutokana na virusi vya corona.
Hata hivyo Ruto alisema kuwa BBI haipaswi kuzingatia vyeo vya wanasiasa bali yapaswa kuzingatia hali ya mwananchi wa kawaida.
“Reggae itasimama, haitasimma? Itasimama, wawache kiburi bwana. Msituambia ni lazima na msituambia ya kwamba nobody can stop reggae, Kuna mungu mbinguni na kuna wananchi hawa. Kama Mambo ya wananchi hawa haiku kwa BBI, hiyo Reggae itasimama, ama mnasema aje? Hawa watu watajua hajui,
Tumeona BBI imejazwa mambo ya wadosi. Iko na mambo ya Prime Minister, Imperial President na mambo ya vyeo ya wakubwa. Hatuna shida na hiyo lakini lazima kuwe na mambo ya biashara na kazi ya huyu mwanainchi wa hapa chini." Ruto Alisema siku ya Jumapili.
Kwa upande huu mwingine Uhuru na Raila wamewauliza wananchi wa kenya kuunga mKono BBI baada ya kujisomea na kuamua uamuzi wao.
Raia anatarajiwa kuongoza zaidi ya wakenya 6,000 ambao wamealikwa katika uzinduzi wa BBI katika ukumbi wa Bomas.
Kulingana na ratiba ya hafla hiyo ya leo baadhi ya viongozi ambao wanatarajiwa kuzungumza ni naibu mwenye kiti wa kamati ya BBI Adms Oloo na kinara wa ODM Raila Odinga.
Mnamo mwaka wa 2019,Novemba,27 Ruto alikuwa kwenye vichwa vya habari baada ya madai kuwa alitumiwa vibaya wakati wa uzinduzi wa kawaida wa BBI.