Wabunge wanaowaunga mkono rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga wamesema wako tayari kwa kura ya maoni kuhusu mapendekezo ya ripoti ya BBI .
Wajumbe hao kutoka senate na bunge la kitaifa wamesema wametathmini yaliyomo katoika ripoti hiyo na kuamua kuiunga mkono .
Hii ni baada ya wabunge hao kufanya kutano na rais Uhuru na kiongozi wa ODM Raila huko Naivasha .
Wakiongoziwa na seneta wa Siaya James Orengo ,viongozi hao wamesema wako tayari kulisaidia taifa kuafikia umoja ambao unahimizwa kupitia mapendekezo ya BBI .
Amesema kupitia kuongezwa kwa fedha za kaunti hadi asilimia 35 ,kaunti zitakuwa na raslimaliza kutosha kutoa huduma kwa wananchi .
Oreng amesema mswada wa BBI utahakikisha kwamba kesi za uhalifu wa kiuchumi na ufisadi zinashughulikiwa ndani ya kipindi cha miezi sita .
Orengo amesema mkutano wao umeunga mkono pendekezo la kuunda nafasi zaidi za uakilishi ili kukimu mahitaji ya wanawake ,vijana na makundi yaliyotengwa .
" Tuko tayari kuendelea na jitihada za kuhakikisha kwamba kilele chake ni kuandaliwa kwa kura ya maoni’ amesema Orengo .