Kwa kawaida unapoenda kupatana na mpenzi wako kwa mara ya kwanza lazima heshima idumu kwa maana hajaweza kuzoeana sana.
Kuna mambo ambayo wengi hawatilii maanani huku baada ya kupatana unawachwa na siku hiyo bila hata ya kufahamishwa wala kuambiwa chochote.
Haya basi msitie shaka kama mwanamume au mwanamke unapaswa kutilia mambo haya maanani wakati wa uchumba wako wa kwanza.
1.Kutaniana na watu wengine
Unapo pata umepelekwa katika mkahawa ambao unaufahamu na kuwa kuna watu unawafamu kuwa makini na uchumba wako na wala usiweze kutaniana na watu wengine.
Hiyo ni njia moja wapo ya kuonyesha kuwa huna maana na uhusiano ambao mnaenda kuunda na atakaye kuwa mpenzi wako.
2.Kutuma jumbe wakati mko pamoja
Kama umeamua wakati huo ni wenu wawili haya basi weka simu kando na uwe makini na kile mwenzako anachosema.
Simu ndio huwa nayo kila mara kwa hivyo mwenzio ni kwa muda tu uwe naye kisha muachane.
3.Kutokuwa wewe mwenyewe
Kama hujazoea kula vizi karai ambia mwenzako kuwa hutaki viazi karai umezea kula ugali na vitu vingine.
Kama ni mavazi valia mavazi yako usiweze kuomba mwenzio usije ukajitia aibu mbele yake.
4.Kuzungumzia yaliopita
Wacha uhusiano au mambo ya awali yawe ya awali huo si wakati mwafaka wa kuzungumzia mambo kama yale zungumzia mambo yaliyomo na yatakayo kuwa.
5.Kutia macho katika simu ya mwenzio
Kuna wale lazima watazame nini mwenzake anachokifanya katika simu yake haya basi muache afanye anacho fanya na wala si kupeleka shingo na macho kwenye simu yake.
Na tumai umesoma mawili aua matatu.

