Msanii wa nyimbo za kikuyu Betty Bayo ameamua kufunguka zaidi kuhusu maisha yake na hasa changamoto ambazo amezipitia mwaka huu wa 2020 .
Bayo amesimulia jinsi alivyokabiliana na hali ngumu kimaisha tangu alipomuacha mume wake wa zamani Victor Kanyari ,akisema kwamba amepotteza gari lake ,nyumba na zaidi ya yote ndoa yake .
Mama huyo wa watoto watatu amesema miaka mitao iliyopita alipokuwa ‘celeb’ nusura asalimu amri kwa sababu kila alichopenda kilitoweka
Amesema kwamba hali ilikuwa ngumu kwake na kuweza kuudu hata lishe bora kwa watoto wake
“ Nakumbuka sikuweza hata kuwalisha wanangu lishe bora …. Nilikosa kulipa kodi ya nyumba kwa miezi sita na mfanyikazi wangu wa nyumbani lakini alisalia mtulivu .Sikutaka kumuambia yeyote akiwemo mamangu kuhusu kilichokuwa kikifanyika kwa sababu wengi hawangeamini…marafiki wengi waliniacha’ amesema Bayo.
Amesema kilichompa nguvu ya kuendelea kuishi ni Imani yake kwa mola na hakuacha kuomba ili hali iboreke . Betty amekuwa akifunguka kuhusu mengi katika miezi ya hivi karibuni huku akitoa ushauri wa ndoa kwa wanawake mbali mbali kupitia mtandao