Vijana,18,walikamatwa na polisi katika kaunti ya Kiambu huku wakufanya sherehe kinyume cha kanuni za virusi vya covid-19.
Kulingana na polisi vijana hao walikuwa kati ya miaka 16 na 18 walikuwa wanasheherekea siku ya kuzaliwa na mmoja wao ambapo walikuwa wanabugia vileo.
Kulingana na citizen Digital, DCC wa Ruiru Githinji Geoffrey alisema kwamba vijana hao walikuwa wamekusanyika eneo hilo kinyume na kanuni za wizara ya afya na waliowauzia pombe watakamatwa.
Pia aliwauliza wazazi wawe makini na mahali watoto wao wako hasa wakati huu shule zimefungwa na asilmia kubwa ya wanafunzi wako nyumbani.
DCC Githinji alisema kuwa watoto hao wataachiliwa kwa wazazi wao mnmo siku ya Jumamosi.
Haya yanajiri siku chache baada ya vijana zaii ya arobaini kukamatwa wakiwa wamefungiwa nyumbani na wakibugia vileo huku polisi wakipata kondomu zilizotumiwa.
