Jamaa,familia na marafiki wa Steven Munga almaarufu hawajaweza kuamini kuwa ameaga dunia kutokana na kichapo ambacho alipokea kutoka kwa walinzi mlango katika tamasha la Nai Fest tarehe 7,Novemba.
Ni tamasha ambayo ilikuwa imeandaliwa na mwanasosholaiti Bridget Achieng.
Kijana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya upili ya Mukaa hakurejea nyumbani kwao siku hiyo huku simu yake ikizimwa.
Kulingana na mpasho mwili wake ulipatikana kwenye kuchamba cha kuifadhi maiti siku tano baadae.
"Tumekuwa tukimtafuta kwa siku tatu, tumeenda katika vituo vya polisi kadhaa, hospitali na hata vyumba vya kuifadhi maiti
Tulimpata baadaye katika chumba cha kuifadhi maiti jijini Nairobi, kichwa chake kilikuwa kimebondwa na jicho lake limedungwa."Baba yake aliambia vyombo vya habari
Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mpenzi wake aliandika ujumbe wa kumuomboleza huku akisema kwamba anampenda sana.
"Nakupenda sana, cheza na malaika huko juu 🥺🥺RIP…" Aliandika mpenzi wake Shanty.
kupitia katika posti nyingine aliandika,
"RIP BABE😪😪."
Pia baba yake alisema kwamba marafiki zake waliokuwa nao walisema kwamba alirudi bila shati na viatu vyake, hii ni baada ya kuambiwa kuwa yeye ni mwizi.