Siku chache baada ya msanii Diamond kutoa kibao chake kipya cha 'Waah' wakenya walimuunga mkono huku rappa Octopizzo akighadhabishwa na kitendo hichona hata kuwakashifu.
Siku chache baada ya ukashifu wake Otile Brown ameweza kuzungumza na kusema kila mtu ana haki ya kuunga na kupenda kibao ambacho anataka au msanii ambaye anataka.
Kupitia kwenye ukrasa wake wa twitter Otile alikuwa na haya ya kusema;
"Sadieni msanii ambaye mnataka, unga mkono chochote ambacho unataka na unapenda, muziki hauna mipaka, wivu ni ishara ya udhaifu na sio yetu
ata ukitaka leta ushindani wako chini, huwezi lazimisha watu wapenda ujinga wako, sina jambo lolote dhidi ya wasanii wa humu ata wanchi za nje ni upendo tu
Wakati mwingine naweza kuwachukia laini si jambo la kibinafsi, hii ni burudani tu, ndugu yetu anastahili hili alifanyia kazi haya
Ninaheshimu wasanii wote licha ya nyimbo zipi wanaimba, kama inaleta pesa basi ni sawa, tuwache kunung'unika kibuma turudi jikoni kwa vyombo vyetu vya habari endeleeni kutuunga mkono
Si tu wasanii wale maarufu zaidi au nyimbo kali..kama wimbo ni mzuri peana shavu ata kama ni msanii chipukizi
Ni sawa kamahautapenda muziki wangu au kuunga mkono." Otile Brown Aliandika.
