Msemaji wa timu ya mpira ya Msimbazi maarufu Simba FC Manara amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa miaka mingi.
Harusi yake ilihudhuriwa na marafiki wa karibu, wanakandanda, wanasiasa na familia kutoka pande zote mbili.
Msanii na staa wa bongo nchini humo Diamond Platnumz hakuhudhuria harusi yake licha ya kuwa rafiki wa karibu wa Manara.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikuwa na haya ya kusema kuhusu harusi hiyo.
" My brother @hajismanara roho imeniuma sana kukosa katika siku yako hii kubwa kutokana na mambo ya kazi...lakini naamini Mwenyez Mungu ana Mipango yake...najua now mnaenda Honeymoon mkirudi tafhadhali naomba wasaa nije kuwatembelea nyumbani, nami niwaletee kizawadi changu...Hongera sana na Mwenyez Mungu awajaalie Ndoa yenye Upendo, Maskilizano, Amani, Mafanikio na Kudumu🙏🏼." Aliandika Diamond.
Diamond alisema kwamba alikosa kuhudhuria harusi hiyo kwa maana alikuwa na shughuli za kikazi.
