logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KEBS yaidhinisha viwango vya ubora vya uzalishaji wa wadudu wa kuliwa

Viwango hivyo vya ubora  KS 2921:2020 vimetoa mahitaji ambayo yanafaa kutoshelezwa  na wakulima ikiwemo hali itakayofanikisha uzalishaji na uuzaji wa wadudu hao ili kutumiwa kama chakula

image
na Radio Jambo

Habari14 December 2020 - 17:05

Muhtasari


  • Viwango hivyo vya ubora  KS 2921:2020 vimetoa mahitaji ambayo yanafaa kutoshelezwa  na wakulima ikiwemo hali itakayofanikisha uzalishaji na uuzaji wa wadudu hao ili kutumiwa kama chakula
  • KS 2922 Part 2   ni mwongozo utakaotumika kuunda bidhaa zinazotokana na wadudu hao kama vile biskuti  na bidhaa nyingine .

 Halmashauri ya kukadiria ubora wa bidhaa KEBS imeidhinisha viwango vya ubora vitakavyotumiwa  kuongoza uzalishaji wa wadudu wanaoliwa na bidhaa zinazotokana na wadudu hao .

 Viwango hivyo vya ubora  KS 2921:2020 vimetoa mahitaji ambayo yanafaa kutoshelezwa  na wakulima ikiwemo hali itakayofanikisha uzalishaji na uuzaji wa wadudu hao ili kutumiwa kama chakula . Pia vinatoa kiwango kinachohitajika cha miundo msingi inayohitajika kwa uzalishaji wa wadudu kwa wingi .

 Maneja mkurugenzi wa KEBS Bernard Njiraini amesema  KS 2922 Part 1  ni mwongozo utakaoeleza na kuratibu mahitaji ya kupakiwa na kuuzwa kwa wadudu hao wakiwa wazima ama wakisagwa .

KS 2922 Part 2   ni mwongozo utakaotumika kuunda bidhaa zinazotokana na wadudu hao kama vile biskuti  na bidhaa nyingine .

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved