Wikendi iliyopita marafiki wake mwendazake Charles Bukeko almaarufu Papa Shirandula wikendi iliyopita walisheherekea sikukuu ya Jamhuri kwa njia ya kipekee.
Hii ni baada ya marafiki hao kutembelea familia yake katika kaunti ya Busia.
Wengi hawakufahamu sababu ya marafiki hao kuenda eneo hilo bali aliyekuwa muigizaji wa kipindi hicho Jackline Nyaminde almaarufu kupitia kwenye ukurasa wake alifichua sababu ya wao kuenda huko.
Huku akipakia picha ya Njoro,Awinja naye liandika ujumbe huu;
" Ni wikend ya ajabu aje, kurudi Nanderema, Samia kaunti ya Busia kutembelea familia ya Papa na wazazi wake na eneo ambalo tulimzika
Kijiji chote kilikua na nilisikia vizuri, ilikuwa sherehe,tuliimba,tukasakata densi, tukakula na tukakunywa ni ahadi ambayo tulifanya wakati wa mazishi yake tutarudi tena
Tunafuraha kwa maana tulitimiza ahadi hiyo, wazazi wake na familia yake walijawa na furaha na mioyo yetu ilikuwa imejaa." Aliandika Wilbroda.
Wakati huo huo muigizaji mwenzake Jacy Vike almaarufu Awinja alimtambulisha nduguye Papa kwa mashaibiki.