Msimu huu wa krismasi baadhi ya watu wengine huwa furahisha wapenzi wao na zawadi chungu nzima.
Wakati huu wanawake wengi hutarajia zawadi kutoka wa wanaume na wapenzi wao.
Lakini wakati huu wanawake wanapaswa kuwanunulia waume wao zawadi na kuwafurahisha.
Zawadi si zawadi tu bali soma baadhi ya zawadi ambazo unapaswa kumnunulia mwanamme wako kama mwanamke msimu huu wa krismasi.
1. Saa nzuri yenye umaridadi
Ndio kuna saa ambazo ni saa lakini wanaume wanapenda kuvalia saa kwa ajili ya umaridadi wao
Kama mwanamke mtafutie mumeo au mpenzi wako saa nzuri.
2.Viatu
Tafuta kiatu cha mtindo wa sasa mpelekee mpenzi wako msimu huu wa krismasi, na utaona mapenzi yenu yakinoga kunoga.
3.Mnunulie simu nzuri
Kuna aina nzuri za simu ambazo zimezinduliwa hivi karibuni, mbali na kuwa na simu ambayo ako nayo atakuwa akitumia simu hiyo na kukuona hapo kwa maana ni wewe ulimnunulia.
4.Mashine ya kuosha
Kwa kawaida wanaume wengi ni wavivu kwa kufua nguo na hata kusafisha nyumba zao kama mpenzi wake unaweza mnunulia mashine hiyo.
Zawadi zingine ni kama vichwa vya sauti, kama umebarikiwa na pesa pia unaweza mnunulia gari.
Unaweza mnunulia mpenzi wako zawadi ipi wakati huu wa sikukuu?