logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uhuru azuru Kisumu, akagua ujenzi wa uwanja mpya wa michezo

Uhuru azuru Kisumu, akagua ujenzi wa uwanja mpya wa michezo

image
na Radio Jambo

Habari10 January 2021 - 14:28

Muhtasari


  • Rais alitembelea eneo la Mamboleo , ambapo ujenzi wa uwanja wa Kimataifa wa michezo wa Jomo Kenyatta unaendelea.

  • Uwanja huo ulipaswa kujengwa katikati mwa mji wa Kisumu, lakini hapakuwepo nafasi ya kutosha.

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumapili alitembelea eneo la Mamboleo ASK, ambapo ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa michezo wa Jomo Kenyatta unaendelea.

Baada ya kuhudhuria mazishi ya mama mzazi wa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi siku ya Jumamosi Rais alisalia magharibi na kulala katika ikulu ndogo ya Kisumu.

Uhuru alitembelea eneo la ziwa Victoria mwishoni mwa mwezi Oktoba kukagua mradi wa ujenzi unaoendelea katika eneo la Mamboleo na ambao unatarajiwa kuchukua miezi sita kukamilika.

 

Uwanja huo ulipaswa kujengwa katikati mwa mji wa Kisumu, lakini hapakuwepo nafasi ya kutosha.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga alisema mradi huo ulihamishwa kutoka katikati mwa mji wa Kisumu kwa sababu ya ukosefu wa nafasi ya kutosha kuchukua watu wengi wakati wa hafla kubwa ya  kispoti.

Alisema mradi huyo ukikamilika itatoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana katika eneo hilo na kuongeza kwamba kuwapa vijana pesa kila wakati sio suluhisho kwa vijana kukosa ajira.

Mradi huo ulianzishwa na Waziri Amina Mohammed.

Eneo la ujenzi lilikabidhiwa kwa wakandarasi wiki iliyopita katika hafla iliyoongozwa na Gavana Anyang 'Nyong'o na Naibu Katibu katika Wizara ya Michezo Josephine Onunga.

Uwanja huo wenye uwezo wa mashabiki 30,000 utakuwa na eneo la mpira wa soka, raga, tenisi, magongo miongoni mwa fani zingine.

"Tunaunda uwanja wa kimataifa hapa Mamboleo na aina hii ya barabara haipaswi kuongoza watu kwa uwanja huo," rais Kenyatta alisema.

 

"Nitakuja hapa Aprili mwaka ujao na hii inapaswa kuwa imekamilika wakati huo."

Miezi minne iliyopita, serikali iliidhinisha Shilingi bilioni  4.9 kwa ujenzi wa barabara hiyo baada ya miongo miwili ya kutelekezwa.

Barabara hiyo, ambayo iko katika hali mbaya, inaunganisha Kisumu na kaunti jirani.

Rais Kenyatta pia alikutana na magavana wa kanda ya magharibi  wakiwemo Wycliffe Wangamati (Bungoma), Wycliffe Oparanya (Kakamega), Sospeter Ojaamong (Busia) na Nyang Nyong'o (Kisumu) miongoni mwa viongozi wengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved