logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond afunguka kuhusu utata wa ni nani baba yake wa kumzaa

MAMAKE ALIKUA HANITAKI KABISA AND MZEE ABDUL PIA ALIKUA AMENIEKA MBALI HADI KIPINDI HICH NAKUMBUKA AKINIAMBIA, ‘UMETUMWA NA MAMAKO UJE UNIANGALIE KAMA NAFA, SIFI MIMI.’

image
na Radio Jambo

Football29 January 2021 - 05:01

Muhtasari


  • Akizungumza katika mahojiano na Wasafi Radio, Diamod amesema licha ya kuishi vizuri na mzee Abdul ambaye awali alifahamika kama baba yake, lakini aligundua kuwa baba yake mzazi ni mzee Nyange ambaye kwa sasa ni marehemu.
  • 'Kama niliukataa ujauzito, iweje nimlee Diamond miaka yote hiyo? alihoji Mzee Abdul ambaye alimlea Diamond tokea akiwa mdogo na watu wengi kudhani kuwa ndiye baba yake mzazi.

 

  Staa wa muziki wa Tanzania  Diamond Platnumz,ameweka wazi siku ya alhamisi  ukweli kuhusu baba yake mzazi.

Akizungumza katika mahojiano na Wasafi Radio, Diamod amesema licha ya kuishi vizuri na mzee Abdul ambaye awali alifahamika kama baba yake, lakini aligundua kuwa baba yake mzazi ni mzee Nyange ambaye kwa sasa ni marehemu.

''Nikiwa na kama miaka 11 hivi niliambiwa na mmoja wa majirani zangu kwamba nenda pale kwenye soko la Tandale, halafu muulizie Salum Bubu au Iddi Nyange, nikafika akanipa shilingi mia mbili na mchele, kwa sababu alikua anauza mchele wa ujumla'' Alisema Diamond.

 
 

''Mwanzoni nilikua naona utofauti kwenye vitu vingi, lakini sikuweza kuelewa baadhi ya vitu kwa sababu ya utoto'' Aliongeza Diamond.

Takribani wiki mbili zilizopita, nchini humo kulikuwa na gumzo mtandaoni kuhusu baba aliyefahamika kama mzazi wake Diamond kuwa si baba halisi wa mwanamuziki huyo.

Gumzo hilo lilianza mara baada ya mama yake Diamond kuongea kwenye radio kuwa baba ambaye anadai Diamond amemtelekeza si baba wa kumzaa, baba yake Diamond ni marehemu na alikuwa anaitwa Nyange na si Abdul.

 ‘Ukiamuangalia Diamond na Ricardo unaona nini? ..

  babake ricardo ndiye babake Diamond  na jina lake ni Salum Iddi’

  Mtangazaji Dida alijibu kwamba wawili haoa walikuwa wakifanana .

Mama huyo aliweka picha ya Diamond ikiwa pamoja na Nyange, kuonesha jinsi wanavyofanana.

 
 

Hatua hiyo imeendelea kuzua mijadala katika mitandao ya kijamii nchini humo, haswa baada ya baba anayedai kuwa ndiye mzazi wake ''Abdul'' kutoridhishwa na tukio hilo kwa madai ya kwamba aliukataa ujauzito.

''Kama niliukataa ujauzito, iweje nimlee Diamond miaka yote hiyo? alihoji Mzee Abdul ambaye alimlea Diamond tokea akiwa mdogo na watu wengi kudhani kuwa ndiye baba yake mzazi.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved