logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila kuandaa kikao cha BBI Kisumu baada ya mkutano wa Uhuru Sagana

Mkutano huo wa Raila utafayioka wiki moja baada ya rais Kenyatta kuandaa mkutano Sagana na viongozi kutoka mlima Kenya kuwashawishi waunge mkono mswada wa BBI

image
na Radio Jambo

Habari30 January 2021 - 06:29

Muhtasari


  •   Mkutano huo wa Raila utafayioka wiki moja baada ya rais Kenyatta kuandaa mkutano Sagana na viongozi kutoka mlima Kenya kuwashawishi waunge mkono mswada wa BBI .
  • Katika mkutano wa Kisumu  Raila atakutana na  magavana wote ,wabunge ,wataalam na waakilishi wa mabunge ya kaunti kutoka  Migori, Homabay, Kisumu  na Siaya.

 

Rais Uhuru Kenyatta  na kiongozi wa ODM Raila Odinga wameamua kurejea katika ngome zao kupigia debe ripoti ya BBI baada ya  mswada wa BBI kuidhinishwa na tume ya uchaguzi nchii IEBC .

 Kiongozi  huyo wa ODM  anapanga kufanya mkutano mkubwa na washika dau katika sekta mbali mbali  kutoka kaunti nne za Luo Nyanza februari tarehe 8  huku BBI ikitarajiwa kuwa ajenda kuu .

 Mkutano huo wa Raila utafayioka wiki moja baada ya rais Kenyatta kuandaa mkutano Sagana na viongozi kutoka mlima Kenya kuwashawishi waunge mkono mswada wa BBI .

Uhuru  amekuwa katika eneo la kati tangu siku ya ijumaa  katika kile ambacho ikulu imetaja kama ziara ya kikazi na  ya kukutana na viongozi waliochaguliwa kutoka eneo hilo ili kujadili BBI na masuala mengine yanayohusu maendeleo .

 Katika mkutano wa Kisumu  Raila atakutana na  magavana wote ,wabunge ,wataalam na waakilishi wa mabunge ya kaunti kutoka  Migori, Homabay, Kisumu  na Siaya.

 Mkutano huo pia utawahusisha waakilishi wa kibiashara  na wazee wa jamii ya Waluo , Tayari mialiko imetumwa kwa takriban watu 800  .

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved