Iwapo umefikiri makali ya januari yamekuacha hoi basi kuna fursa ya kujishindia pesa kilao uchao katika mchezo mpya utakaoendeshwa na Mtangazaji Shaffie Weru , Happy Hour Bar Quiz na unaweza kujisajili Nikoplay.co.ke.
Show bombaa inaanza tarehe 5 februari kuanzia saa sita mchana na utakuw ana dakika tano kujibu maswali mboha kabisa ili kujizolea hela.
Mtangazaji huyo amesema ;
“ Ukitaka nikulipie bili zako hakikisha umejisajili ,mtu yeyote anaweza kushinda na maswlai yatahusu mambo ya kawaida kama vile burudani ,udaku-na kila kitu ambacho watu huzungumzia katika baa’
Ameongeza kusema ;
“ Hutozwi chochote na unahitaji tu kuwa na simu ya mkononi na pindi tu show inapofika tamati na umejibu maswali ipasavyo utakuwa na hela zako mkononi’
“ Nataraji nitaweza kuwapa watu hadi shilingi laki moja kwa wakati lakini kwa sababu ndio mwanzo ,nitatadondosha shilingi elfu 20’
Iwapo umesalia mfuko kibogoyo na una ustadi kuweza kumpiku Shaffie ,fursa ndio hii ya wazi ….jisali sasa!