Alfred Musambi alijiona mjinga wa shule lakini hakujua maisha yamemtayarishia mshutuko wa kuonekana hata mjinga Zaidi .
Mapenzi haya ya kuanzia shule ya upili kwake yalionekana kama yatakayodumu na baada ya kupoteleana na Isabel wakati kila mmoja alipohamia mji mwingine baada ya shule ya upili ,ilikuwa bahati sana walipopatana tena kupitia mitandao ya kijamii . walipojikumbusha maisha yao ya shuleni kama wapenzi ,waliamua kuendeleza mambo walipoyaachia na ndipo uamuzi wa Isabel kuja kuishi nan a Alfred mjini Mombasa ulipozua makubwa .
Isabel akahamia Mombasa kutoka Wote ,huku akijua fika kwamba uhusiano wake na Alfred ulikuwa umepangwa tangu jadi na mola na utaishia kuwa ndoa . Jambo ambalo hakuwa amejikumbusha ni kuhusu uhusiano wake na mwanamme mmoja wakati huo pale Wote ambao hakuwa tayari kuusalimisha . Ikawa sasa Isabel anadona pawili –hataki kumucha mpenzi wake mpya wala kumuacha yule Alfred ambaye walikuwa wamefufua mapenzi tena .
Msichana akajiona stadi kwamba ataweza kucheza kama sogora na hivyo baada ya kwenda Mombasa wakaanza kuishi na Alfred katika nyumba moja .Muda usio mrefu , mpenzi wake Isabel wa kutoka Wote anaye pia alisafiri kwenda Mombasa kuishi katika nyumba ile ile ,ikawa wamepanga njama ya kumdanganya Alfred kwamba walikuwa binamu kwamba mtu na Cousin yake sasa huwezo kuingilia wala kushuku lolote .
Wakati Alfred alipokuwa amekwenda kazini ,aliwaacha chumbai pale mtu na mpenzi wake ambao walifanya yote waliotaka . Wakati mwingine mchana , yule mpenzi wa pili alikuwa akitoka kwenda mjini kutafuta kazi lakini majirani waligundua mambo ya kushangaza kwa sababu walishuhudia kwamba Isabel alikuwa kaishi na wanaume wawili na mmoja hakuwa jamaa yake kama alivyodai kwa sababu mchana peupe walikuwa wakijifungia chumbani na kufanya mambo yao kabla Alfred hajarejea .
Kwa sababu daku daku za baadhi ya majirani hazifichiki ,mmoja alipata ujasiri kwa kumuambia Alfred kuhusu kilichokuwa kikifanyika .Mtego uliwekwa na kama inavyotajiwa ,ilibainika wazi wazi kwamba mtu na cousin yake walikuwa ni Isabel na mpenzi wake ambao walikuwa wakimdoea Alfred kwa kuishi kwake ,kula vyake na kumhadaa ilhali walikuwa wakijua wanachofanya .
Ilichukua nguvu za polisi kuzuia maafa pale kwa sababu hasira za Alfred hazikuweza kutulizwa hata na majirani waliomtaka awe mtulivu wakati Isabel na ‘Cousin’ yake walipokuwa wakifungisha virago vyao kuondoka kutoka chumba chake . Yaani walimwengu hawana stara ,peupe machoni unahadaiwa kimapenzi bila kujua .
Je,unawajua binamu za mpenzi wako? Chunga sana !