logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sijawahi ona ngozi nyeusi katika kitabu cha watoto,'Lupita aeleza kwanini aliandika kitabu cha Sulwe

Lupitia alifichua kwamba akiwa na miaka mitano alifikiri kwamba kuna kitu mbaya na ngozi yake.

image
na Radio Jambo

Habari21 February 2021 - 07:08

Muhtasari


  • Lupita afichua sababu ya kuandika kitabu cha Sulwe, huku akisema kwamba hajawahi ona ngozi nyeusi kaika kitabu cha watoto
lupita-nyongo1

Lupita Nyong'o akiwa kwenye mahojiano kwenye mitandao ya kijamii ya instagram na msanii Estehr Akoth almaarufu Akothee alipeana sababu yake ya kuandika kitabu cha Sulwe.

Lupitia alifichua kwamba akiwa na miaka mitano alifikiri kwamba kuna kitu mbaya na ngozi yake.

Mara kwa mara alijaribu kubadilisha rangi ya ngozi yake akiwa Nairobi, wakati huo alikuwa ameolewa, alithibitisha Lupita.

 

"Nilijaribu kubadilisha rangi ya ngozi yangu baada ya kuona wamama wenzangu wakiwa na rangi tofauti na yangu, nilichoelewa ni kwamba watu wa kutoka upande wetu ni weusi kwa ajili ya jua nyingi,"

Huku akizungumzia maisha yake na kuandika kitabu cake alikuwa na haya ya kusema,

'Nilipkuwa nakua nilipokea kejeli nyingi kwa sababu ya rangi ya ngozi yangu, kuna dada yangu ambaye alizaliwa nyuma yangu na alikuwa mweupe alipokea sifa nyingi kutoka kwa shangazi,wajomba na hata marifiki zangu jinsi ni mrembo lakini sikusifiwa

Nilipofika miaka mitano na kugundua kwamba nina ngozi tofauti kuliko wale wengine, nilianza kufanya mambo mengi ambayo, yalikuwa yanafanywa na Sulwe kwenye kitabu,"

Lupita alikiri kwamba hajawahi ona ngozi nyeusi katika kitabu cha watoto, na ndio maana aliandika kitabu hicho kuwashauri watoto kwamba ni warembo mbele ya ulimwengu.

"Sijawahi ona ngozi nyeusi katika kitabu cha watoto, ndio maana niliandika Sulwe ili kuwahimiza watoto kwamba ni warembo mbele ya ulimwengu

Ukiwa mchanga kabla ya dnia, wazazi kukuambia wewe ni nani una fuersa ya kutambua thamani yako ulimwnguni," Aliongea Lupita.

 

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved