Hawakukosea waliposema kwamba uzuri bila maadili mema hauna maana. Hakuna furaha kuwa na mpenzi mzuri ambaye hana maadili.
Wanawake wengi wanafanyiwa upasuaji na hata kupidoa ili waweze kupendwa na wapenzi wao zaidi na zaidi kila siku.
Lakini kuna wale hawana maadili mema, bora wanajua tu ni warembo na wanawamaliza wanaume humu nje.
Urembo hautoshi, kwa maana kuna sifa ambazo wanaume ambao wamefungua macho.
Hizi hapa baadhi ambazo wanaume utafuta kwa mwanamke.
1. Kupika
kwa kweli wazungu walisema 'The way to a mans heart is through his stomach' kama kwa kweli wewe ni mrembo ilhali hujui kupika wala kumfurahisha mpenzi wako kupitia kwa chakula chako wewe si mrembo.
Pia wanaume waangalia kama mwanamke anajua kupika.
2.Heshima
Kama wewe huna heshima kwa wanaume haya basi utazidi kujipodoa na hutapata mwanamume au mpenzi wa maisha yako.
3.Dini
Kuna baadhi ya wanaume ambao wataangalia kama mwanamke ana mtumikia Mungu ipasavyo, na wala hatamchumbia wala kumuoa mtu ambaye hana heshima kwa Mungu wala hapendi mambo ya Mungu
4.Bidii
Karne hii ya sasa kila mwanamke anapaswa kuwa na bidii na wala sio kuamka na kukaa tu kwa nyumba anangoja pesa za mwanamume.

