Mcheza santuri George Njuguna almaarufu DJ Creme De La Creme kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kwamba amemvisha mpenzi wake na mama wa watoto wake pete ya uchumba.
Wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapaenzi kwa zaidi ya miaka kumi, huku wakiwa wamebarikiwa na watoto wawili.
Kupitia kwenye ukurasa wake alipakia picha ya mpenzi wake akiwa amevalia pete hiyo na kuandiika ujumbe ufuatao,
"Ilinichukua miaka 14, kumuuliza rafiki yangu bora,msiri wangu,mama wa watoto wangu, mtu wangu wa milele aweze kunioa
Najua nilikupa mawazo mengi lakini nataka ufahamu moyo wangu na kila kitu changu ni chako nataka kukupenda milele,"
Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki,
anitanderu: Congratulations to you bothπΎπππ
talliaoyando: Congratulations ππΎ
millychebby: Congratulations ππππ
djmzito: Congratulaions bro all the best
chriskirwa: Wow awesome π πππ Congratulations @thecremedelacreme and @deekingsky πβZawadi will decide dress code ππ kwisha Nyinyi