Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa akiwa kwenye mahojiano na runinga moja humu nchini siku ya Jumanne, Machi 16 alisema kwamba hendisheki ilikuwa faida kwa rais Uhuru Kenyatta na wala sio kwa nchi nzima wala Raila Odinga.
Usemi wake unajiri baada ya hendisheki kufikisha miaka mitatau, na baada ya James Orngo kudai kwamba kuna watu ambao wamo serikalini wamepanga kumtema Raila Odnga.
"Nataka kusema ukweli na wacheni kuwadanganya wananchi wa Kenya. hendisheki ilikuwa faida kwa Rais Uhuru Muigai Kenyatta
Lakini haikuwa faida kwa Raila Odinga wala nchi nzima. Mpango huo umekwisha, na ndiyo sababu ana mpango wa kumtema na kumuacha Raila Odinga kama alivyofanya kwa DP William Samoei Ruto. " Alizungumza Didmus.
Baada ya tetesi hizo baadhi ya viongozi w chama cha ODM wanamtaka Raila kujiunga na naibu William Ruto mbele ya uchaguzi mkuu wa waka wa 2022.