Wenye mikopo ya benki sasa wana miezi mitatu ya ziada kuanza kulipia hiyo baada ya Benki Kuu ya Kenya kuongeza muda huo hadi Julai 3.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne, Benki Kuu ya Kenya ilisema kwamba agizo hili linahusu tu mikopo ambayo ilikuwa ikilipiwa kufikia Machi 2, 2020 lakini ikaingia kwenye malimbikizo baadaye kutokana na athari za janga la Covid-19.
'' CBK itaendelea kufuatilia kwa karibu kufutwa kwa mikopo iliyobadilishwa ili kuhakikisha uthabiti wa sekta ya benki, '' CBK ilisema.
Benki kuu ilifichau kwamba angalau mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.7, inayowakilisha asilimia 57 ya jumla ya mikopo ya benki ili fanyiwa mabadiliko katika mikaba yake ya ulipaji tangu ilipotangaza hatua ya dharura katikati mwa mwezi Machi mwaka jana ili kuwaokoa akopaji kutokana athari za janga la Covid-19.
Hata hivyo, tangu kulegezwa kwa masharti ya udhibiti wa maambukizi ya virusi vya corona, wakopaji walianza kulipia mikopo, na kupunguza mikopo iliyobadilishwa hadi shilingi bilioni 569.3 au asilimia 19.
Angalau asilimia 95 ya wakopaji sasa wanalipia mikopo yao.