logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KQ yazama zaidi katika lindi la hasara

KQ yazama zaidi katika lindi la hasara

image
na Radio Jambo

Habari23 March 2021 - 08:02

Muhtasari


• Hasara iliyosajiliwa na kampuni hiyo iliyongezeka mara tatu zaidi ya hasara iliyosajiliwa kipindi cha mwaka uliyotangulia.  

• Athari za janga la corona zilisababisha kupungua kwa mauzo ya KQ kwa asilimia 60 hadi Shilingi bilioni 52.

Shirika la Ndege  nchini (Kenya Airways) siku ya Jumanne lilitangaza kusajili hasara ya jumla ya Shilingi bilioni 36.57 katika kipindi cha fedha cha mwaka jana.

Hasara iliyosajiliwa na kampuni hiyo iliyongezeka mara tatu zaidi ya hasara iliyosajiliwa kipindi cha mwaka uliyotangulia.  

Ingawa kampuni ya KQ imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kifedha, hali yake iliathirika zaidi kutokana na janga Covid-19, lililopelekea kusitishwa kwa safari zote za ndege kwa kipindi kirefu mwaka uliyopita.

KQ ambayo inamilikiwa kwa kiasi fulani na kampuni ya Air France KLM, ilisema mapato yake yalitumbukizwa zaidi ya nusu katika kipindi cha mwaka jana, baada ya kusitishwa kwa safari za ndege.

Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo  ndege Allan Kilavuka alisema idadi ya abiria ilipungua sana wakati wa kipindi cha fedha cha mwaka jana hadi milioni 1.8 ikilinganishwa na milioni 5.2 mwaka 2019.

Hali hii ilisababisha kupungua kwa mauzo ya KQ kwa asilimia 60 hadi Shilingi bilioni 52.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved