logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Njia za kukabiliana na watu wanaoingilia maisha yako

Kuna baadhi ambao hurudi na nyuma kwa ajili ya maneno ya watu, na wale ambao ukabiliana nao ipasavyo na kuwapa kikomo.

image
na Radio Jambo

Michezo23 March 2021 - 11:05

Muhtasari


  • Katika kila kona za nchi, na kama wewe nimwanadamu lazima kuna kikundi au watu ambao wanapenda kuzungumzia maisha yako na hata kuingilia maisha yako
hook-up-bars-nightclubs-nairobi-meet-women-dating-guide

Katika kila kona za nchi, na kama wewe nimwanadamu lazima kuna kikundi au watu ambao wanapenda kuzungumzia maisha yako na hata kuingilia maisha yako.

Kuna baadhi ambao hurudi na nyuma kwa ajili ya maneno ya watu, na wale ambao ukabiliana nao ipasavyo na kuwapa kikomo.

Je wafahamu njia zozote za kukabiliana na watu ambao wanaingilia maisha yako, na kuchunguza kile unaendeleza katika maisha yako?

Haya basi usitie shaka, hizi hapa njia za kukabiliana na watu kama hao.

1.Jaribu kuchunguza kama wanakutakia mazuri

Kuna wale watu wataingilia maisha yako wakitaka mazuri yakutendekee lakini kuna wale wanataka kukuangamiza milele na kukuona ukilia kila kuchao.

Kama hawakutakii mazuri haya basi jipe shughuli.

2.Weka mipaka

Kuna baadhi ya watu na marafiki ambao hawafahamu wala kujua mipaka katika maisha yako, kuna wale watavuka mipaka na kukuumiza.

Kama una marafiki usiweze kuzungumza na mtu mwingine kuhusu maisha ya rafiki mwenzake weka mipaka na ukatae maneno yake kwa maana yataleta chuki siku moja.

3.Wapuuze

Kuna watu wengine ambao huwezi kuwazuia na lazima udumishe uhusiano wa kiraia nao, kama mwenzako au jirani yako. Ikiwa wataingilia maisha yako, labda ni bora usiwape maanani.

4.Usiwaambie siri zako

Maelezo yako ya kibinafsi huchochea watu wenye ujinga, kwa sababu mara tu watakapojua kitu kukuhusu watataka kutoa maoni juu yake au kuuliza. Kwa hivyo jaribu kuweka mambo  ya kwako, hata ikiwa watakuuliza juu yake nyamaza.

Kuna wale wazee ambao watakuuliza kwanini hujaoa au kuolewa nyamaza na ufanye mambo yako kisiri.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved