logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Orodha ya watoto wa watu mashuhuri waliojizolea alama nzuri katika mtihani wa K.C.S.E 2020

Baadhi ya wanafunzi waliojizolea alama nzuri walisheherekea huku wanafunzi 893 wakijizolea alama ya 'A'.

image
na Radio Jambo

Habari11 May 2021 - 09:37

Muhtasari


  • Siku ya JUmatatu ilikuwa ni furaha kwa watahiniwa wa mtihani wa kidoto cha nne K.C.S.E baada ya matokeo yao kutangazwa na waziri wa elimu George Magoha
NJORO 3

Siku ya JUmatatu ilikuwa ni furaha kwa watahiniwa wa mtihani wa kidoto cha nne K.C.S.E baada ya matokeo yao kutangazwa na waziri wa elimu George Magoha.

Baadhi ya wanafunzi waliojizolea alama nzuri walisheherekea huku wanafunzi 893 wakijizolea alama ya 'A'.

Wanafunzi waliopata alama nzuri walisheherekea kwa njia tofauti huku baadhi ya watu mashuhuri wakiwasheherekea watoto wao waliofanya vyema.

 

Baadhi ya watu hao ni aliyekuwa muigizaji wa kipindi cha Papa Shirandula Njoro, aliyekuwa gavana wa nairobi Mike Sonko, seneta wa zamani Bonnie Khalwale na wengineo.

1.Njoro

Muigizaji huyo alisheherekea mwanawe kwenye ukurasa wake wa instagram huku akifichua kwamba mwanawe alijizolea alama ya B- huku akimshukuru Mungu.

"Asante kwa Mungu, maombi yako hayakuwa ya bure,tumepata alama ya B- najivunia sana sasa jiunge na mimi," Aliandika Njoro.

2.Mike Sonko

NI mwanasiasa ambaye amekuwa akiwasaidia wananchi, huku akijivunia kuwa mwanawe alijizolea alama ya B-

Pia alifichua kwamba katika mtihani wake wa darasa la nane alipata alama  399, huku akijiunga na shule ya upili ya Lenana.

3.Bonnie Khalwale

Mwanasiasa huyo alitangaza matokeo ya mwanawe kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliyejizolea alama ya B+

Hongera kwa watahiniwa ambao walipita mtihani wao wa kidato cha nne, kweli hawakukosea mchumia juani hulia kivulini

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved