Mbunge Moses Kuria wa Gatundu ya Kusini amekiri kuwa yeye ni mmoja wa wabunge waliopokea shillingi laki moja ili kumpitisha Amos Kimunya kuwa kiongozi wa walio wengi bungeni.
Katika mahojiano yake na BBC asubuhi ya Alhamisi, Kuria alikiri kuwa ni kawaida ya wabunge kupokezwa hongo ili kubadilisha misimamo yao na kupitisha hoja bungeni.
“Kiongozi wa walio wengi bungeni alipopitishwa, tulienda kwenye ofisi yake tukatunukiwa hongo ya laki moja kila mmoja wetu” Kuria aliambia BBC.
Alijitetea kwa kudai kuwa angerejesha hongo aliyopokea mwisho baada ya kuulizwa mbona akakubali kupokea hongo ilihali si halali.
Kuria ambaye ni mwandani wake Naibu Rais William ruto alisema kuwa ni dhahiri kuwa mbunge haliwezi kukiri makosa yake.
“Haya mambo hayafanyiki kwa camera na sidhani kamwe wabunge watakubali kuyakiri, lakina yanafanyika sana haswa katika ofisi ya kiongozi wa walio wengi.” Kuria alisema.
Kuria pamoja na Ndindi Nyoro wa Kiharu na Mohammed Ali wa Nyali wameagizwa kufika mbele ya baraza la bunge siku ya Alhamisi kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
Nyoro anakabiliwa na madai kuwa aliwaita wabunge wenzake ‘mauzo’ ilhali Kuria anatuhumiwa kudai kuwa baadhi ya wabunge walipokea hongo kupitisha BBI