logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watengenezaji mikate waonywa dhidi ya kukandamiza wanunuzi

CAK imeamrisha watengenezaji mikate kuandika tarehe ya kuhabika, viungo vinavyotumika na uzani halisi wa bidhaa zao

image
na Radio Jambo

Habari25 May 2021 - 05:50

Muhtasari


•CAK imeamrisha watengenezaji mikate kuandika tarehe ya kuhabika, viungo vinavyotumika na uzani halisi wa bidhaa zao

•Mkurugenzi mkuu wa CAK, Bw. Wang’ombe Kariuki alisema kuwa watengenazaji mikate hawana uhuru wa kuchagua sheria watakazofuata.

mkate

Idara ya kudhibiti ushindani kwenye soko nchini Kenya(CAK) imetoa amri  kali kwa watengenezaji wa mikate nchini.

Kupitia ujumbe kwa wanahabari, idara hiyo imetangaza kuwa hii ni baada ya uchunguzi kukamilika na kuthihirisha kuwa watengenezaji wengi wamekuwa wakikandamiza wanunuzi.

Uchunguzi ulionyesha kuwa watengenezaji mikate hawajakuwa wakiandika tarehe ya kuharibika kwa mikate kwa mtindo uliopeanwa huku wengine wakikosa kabisa kuandika. Inadaiwa kuwa watengenezaji hao hawajakuwa wakiandika uzani halisi na bidhaa zilizotumika kutengeneza mikate hiyo.

Wengine wanadaiwa kuandika kuwa mikate yao imeongezwa vitamini ila hawakusema ni vitamini zipi huku wengine wakishukiwa kudanganya kuwa mikate yao ina maziwa au siagi ya maziwa ila ikabainika wazi kuwa haina.

Kati ya amri zilizotolewa kwa watengenezaji mikate ni pamoja na kuandika tarehe ya kuharibika kwa mikate kwenye karatasi ya kufungia na kuambatanisha na maneno  ‘nzuri kabla’ ama ‘Uza kabla ya tarehe..’

Pia wameagizwa kuandika viungo vilivyotumika kutengeneza mikate na uzani halisi wa bidhaa hizo zilizotumika. Wameamriwa pia kuandika vitamini na madini yaliyotumika.

Mkurugenzi mkuu wa CAK, Bw. Wang’ombe Kariuki alisema kuwa watengenazaji mikate hawana uhuru wa kuchagua sheria watakazofuata.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved