logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize azungumzia orodha ya wasanii iliyotolewa na BET na kuwasihi haya

Harmonize amezungumza baada ya BET kutoa orodha ya majina ambayo ni pamoja na wasanii wa Kiafrika.

image
na Radio Jambo

Habari28 May 2021 - 21:35

Muhtasari


  • BET walitangaza wateule wa 2021 wa tuzo zao. Hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa michezo wa Microsoft, Los Angeles mnamo Juni 27
  • Harmonize alihisi kama tuzo ya akademi ya muziki iliacha mabingwa kadhaa barani Afrika ambao walipaswa kuteuliwa
hamo 3

BET walitangaza wateule wa 2021 wa tuzo zao. Hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa michezo wa Microsoft, Los Angeles mnamo Juni 27.

Megan Thee Stallion na Dababy wameongoza kwa majina saba kila mmoja.

Baadhi ya mabingwa wa muziki wa Afrika walioteuliwa ni pamoja na Davido, Diamond Platinums, WizKid, Burna Boy na wasanii wengine wengi kutoka Afrika.

 Harmonize amezungumza baada ya BET kutoa orodha ya majina ambayo ni pamoja na wasanii wa Kiafrika.

Harmonize alihisi kama tuzo ya akademi ya muziki iliacha mabingwa kadhaa barani Afrika ambao walipaswa kuteuliwa.

Msanii huyo kutoka Tanzania anafahamika sana katika safari yake ya usanii, hadi mahali alipo sasa.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwasihi BET mwaka ujao wasiwaacha mabingwa wa muziki ambao wanafahamika sana Afrika na duniani kote.

"BET najua na nafahamu vile nyinyi huwatambua na kuwatunza mabingwa, tafadhalini mwaka wa 2022 msisahau @si nature na @h.baba," Aliandika Harmonize.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved