logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Shaibu wa miaka 79 aokolewa baada ya kutekwa nyara kwa siku 8

Watekaji nyara walidai kulipwa shilingi milioni mbili ili kumuacha huru Bosire

image
na Radio Jambo

Habari16 June 2021 - 10:11

Muhtasari


•Wasiwasi mwingi ulimpata mkewe Bosire na kumpelekea kuomba usaidizi wa wapelelezi wa DCI.

•Siku nane baadae, wapelelezi waliokuwa wanawawinda waharifu wale waliweza kumnusuru Bosire kutoka mikononi mwa watekeji nyara wanne waliokuwa wamemuzuilia katika nyumba moja kwenye viunga vya mji wa Kitale.

Washukiwa wa utekaji nyara

Maafisa wa polii upande wa Kitale wanazuilia wanaume wawili na mwanamke mmoja wanaoaminika kuteka nyara shaibu wa miaka 79 mnamo Juni 6.

Samwel Atunya, Richard Okari , Grace Kerubo  na Jackson Nyakundi wanadaiwa kuteka nyara mzee kwa jina Kennedy Bosire na kudai malipo ya Shilingi milioni mbili kutoka kwa bibi yake ili kumuachilia.

Imeripotiwa kuwa Bosire alitoweka baada ya ya kuanza safari ya  kutoka Kitale kueleke Kisii mida ya saa kumi na moja unusu jioni ya tarehe Juni 6. Baadae mida ya saa tatu usiku alimpigia bibiye simu na kumuarifu kuwa angelala katika mjini Kitale kabla ya kuelekea Kisii mapema asubuhi iliyofuata.

Bibiye Bosire ameeleza kuwa alipojaribu kumpigia simu asubuhi iliyofuata, simu iliitana ila hakuna aliyejibu.

Baadae mida ya saa mbili unusu siku hiyo alipokea simu geni na kuarifiwa na mtu ambaye hakujitambulisha kuwa walikuwa wameteka nyara bwanake na walidai kulipwa Sh2M ili kumuachilia.

Wasiwasi mwingi ulimpata mkewe Bosire na kumpelekea kuomba usaidizi wa wapelelezi wa DCI.

Siku nane baadae, wapelelezi waliokuwa wanawawinda waharifu wale waliweza kumnusuru Bosire kutoka mikononi mwa watekeji nyara wanne waliokuwa wamemuzuilia katika nyumba moja kwenye viunga vya mji wa Kitale.

Watatu kati ya watekaji nyara wale, Kerubo, Atunya na Okari walitiwa pingu ila mmoja wao kwa jina Jackson Nyakundi hakupatikana.

Pikipiki iliyotumika kumbeba Bosire, gunia na kitambaa kilichotumika kumfunga macho ni baadhi ya vitu vilivyopatikana kwenye eneo la tukio.

Polisi wanaendelea kumuwinda mshukiwa wa nne huku watatu waliokamatwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved