logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Wenye chuki jueni kuna Mungu mbinguni,'Justina Syokau awajibu waliosema ni tapeli

Baada ya siku hcache wengi na wanamitandao walimkejeli

image
na Radio Jambo

Habari24 June 2021 - 11:44

Muhtasari


  • Sijali kuhusu yale mlisema, wenye chuki mnapaswa kujua kwamba kuna Mungu haya ni maneno yake msanii Justina Syokau
  • Justina Syokau awajibu waliosema ni tapeli

Sijali kuhusu yale mlisema, wenye chuki mnapaswa kujua kwamba kuna Mungu haya ni maneno yake msanii Justina Syokau.

Alisema maneno haya kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook, alipokuwa anawakemea na kuwajibu waliosema kwamba ni tapeli.

Mnamo mwezi wa Mei Syokau alivuma sana mitandaoni baada ya kusema kwamba anahitaji msaada wa wasamaria wema ili aweze kulipa bili ya hospitali.

Baada ya siku hcache wengi na wanamitandao walimkejeli na kusema kwamba alikuwa anawatapeli wakenya.

Huku akijibu madai hayo alikuwa na haya ya kusema;

"Wengi walinicheka lakini nimerudi, walienda kwa waganga ili nikuwe mgonjwa lakini Mungu aliniwezesha

Wenye chuki hatuna wakati wenu kwa sasa, mnapaswa kujua kuna Mungu mbinguni, waliniita tapeli lakini nilisaidiwa na watu kutoka nchi za nje na hawakuongea mengi," Alisema Syokau.

Alisema maneno hayo baada ya kuwaambia wanamitandao kwamba anaoa kibao kipya kinachofahamika kama 'NImerudi'.

Kulingana na msanii huyo kibao hicho kinazungumzia ama ni cha kumshukuru Mungu kwa yale amemtendea.

PIa alisema kwamba atazidi kumtukua Mungu na kutingiza kila sehemu ya mwili, kwani biblia inasema kwamba wanadamu wasipomsifu Mungu mawe yatamsifu.

Pia aliweka wazi hatakoma kutingiza sehemu zake za mwili akimshukuru Mungu.

Hii hapa video ya msanii huyo akizungumza;

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved