logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Lala salama!Mbosso aomboleza kifo cha msanii mwenzake

Mwanachama wa bendi alifichua kwamba marehemu alikuwa na shida za shinikizo la damu.

image
na Radio Jambo

Habari24 July 2021 - 07:49

Muhtasari


  • Mbosso aomboleza kifo cha msanii mwenzake
  • Alifariki wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Wananyamala jijini Dar Es Salaam
  • Mwanachama wa bendi alifichua kwamba marehemu alikuwa na shida za shinikizo la damu
  • Mwaka jana, alikuwa amesafiri kwenda India kwa matibabu ya moyo lakini bado haijajulikana ni nini kilimuua
66855938_1220357588125307_5681176959875639446_n

Waziri Ally Kissinger, mwanzilishi wa bendi maarufu ya Kitanzania Kilimanjaro Band maarufu kwa jina la Wana Njenje alifariki jana usiku.

Alifariki wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Wananyamala jijini Dar Es Salaam.

Mwanachama wa bendi alifichua kwamba marehemu alikuwa na shida za shinikizo la damu.

Mwaka jana, alikuwa amesafiri kwenda India kwa matibabu ya moyo lakini bado haijajulikana ni nini kilimuua.

Kupitia kwenye ukurasa wa msanii wa bongi,Mbosso alimuomboleza mwendazake, na kufichua jinsi walikuwa watoe kibao kipya pamoja.

"Daah !! Mzee Wangu Waziri Njenje ..😭 .., Tulifanya wimbo wetu Salama, Tukasafiri Mpaka Tanga na Tukashoot Video Yetu Salama Kabisa na Hivi Juzi tu hapa Tumeongea kwa Furaha kabisa tukiwa tunapanga kutoa Video Ya Wimbo Wetu #Tulizana Leo Umenda Baba .. " Daaah ..

Mwenyezi Mungu Akupe Kauli Thabiti Mzee Wangu , Malaika wa heri Walipambe Kabuli lako Baba 🀲

"Innalillah Wainnailah Raajuun "Hakika Ya Sisi ni Wamwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea πŸ™," Aliomboleza Mbosso.

Bendi ya Kilimanjaro iliundwa zaidi ya miaka 30 iliyopita huko Tanga, Tanzania.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved