logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Naendelea vizuri, muendelee kuniombea" Ringtone azungumzia hali yake na kesi dhidi ya Alai

Ringtone alidai kuwa Alai atasomewa mashtaka siku ya Jumannne

image
na Radio Jambo

Habari26 July 2021 - 07:36

Muhtasari


•Kwenye video iliyoenea sana mitandaoni siku ya Ijumaa Ringtone na Alai walionekena kusababisha drama barabarani huku msanii huyo akiwa amesimama juu ya gari lake aina la Rangerover akiwa anamtetesha Alai kwa kile alisema ni kuchukua sheria mkononi.

•Alai ambaye alikamatwa Ijumaa baada ya tukio hilo aliachiliwa kwa dhamana. Hata hivyo mwanablogu huyo ambaye anatambulika kuwa na sauti sana mitandaoni amebaki kimya kuhusiana na suala hilo.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Ringtone Apoko amewasihi mashabiki wake kuendelea kumuombea huku akiwahakikishia kuwa anaendelea vyema baada ya tetesi kuwa alipigwa kwa rungu na mwanablogu Robert Alai.

Kwenye video iliyoenea sana mitandaoni siku ya Ijumaa Ringtone na Alai walionekena kusababisha drama barabarani huku msanii huyo akiwa amesimama juu ya gari lake aina la Rangerover akiwa anamtetesha Alai kwa kile alisema ni kuchukua sheria mikononi. Apoko alionekana kuvunja damu kwenye upande wa kichwa chake.

Siku ya Jumamosi Apoko ambaye alikuwa na bandeji kwenye uso na mkono wake wa kulia alitangaza kuwa alikuwa ametoka kupokea matibabu  katika hospitali kuu ya Kenyatta na akasema kuwa alikuwa amemshtaki Alai kwa kumvamia. Alisema kuwa angesubiri sheria kuchukua mkondo wake.

Kupitia video aliyopakia kwenye mtandao wa Instagram siku ya Jumapili, Ringtone alidai kuwa Alai atasomewa mashtaka siku ya Jumannne

"Mashabiki wangu wamekuwa wakinipigia simu wakishangaa mbona Robert Alai ameachiliwa. Nataka wasijali Alai atasomewa mashtaka siku ya Jumanne, hakuna kitu anaweza fanya ukatili alionifanyia hakuna mtu anaweza mtetea sheria ya Kenya imeweka wazi" Apoko alisema.

Alai ambaye alikamatwa Ijumaa baada ya tukio hilo aliachiliwa kwa dhamana. Hata hivyo mwanablogu huyo ambaye anatambulika kuwa na sauti sana mitandaoni amebaki kimya kuhusiana na suala hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved