Mumewe waziri wa michezo Amina Mohamed ameaga dunia.
Familia imesema kuwa Khalid Ahmed aliaga akiwa anapokea matibabu katika hopitali ya Karen asubuhi ya Alhamisi baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.
Msemaji wa familia amesema kuwa msiba huo ulitokea mida ya saa kumi na moja asubuhi.
Khalid ambaye ni baba wa wawili hakuonekana sana hadharani kwani alishughulika sana na familia na uendeleshaji wa mabiashara ya familia.
Maafisa waku serikalini walikimbia nyumbani kwa Amina punde baada ya kupokea habari hizo huku mipango ya mazishi ikiendelea.
Familia inasema kuwa waziri Amina ameathirika zaidi kuona kuwa miezi minne iliyopita alipoteza ndugu yake Esmael Mohammed Jibril ambaye alikuwa mwanabiashara ashuhuri nchini.
Jibril aliaga mwezi Machi alipokuwa anapokea matibabu nchini India.
Mengine mengi yatafuata....
(Utafsiri; Samuel Maina)