logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+Picha) Hatimaye Caroline Kangogo azikwa; Familia yatii ombi lake la kuzikwa na gauni ya harusi

Hata hivyo, saluti 21 za bunduki hazikuwepo kama ilivyo desturi katika mazishi ya polisi aliyeaga nchini

image
na Radio Jambo

Habari29 July 2021 - 11:34

Muhtasari


•Mwili wa Caroline ulivalishwa gauni la harusi kama alivyokuwa ameomba kupitia ujumbe wa simu.

•Marehemu pia alikuwa ameomba asizikwe nyumbani kwa aliyekuwa mumewe ila azikwe kwa wazazi wake Elgeyo Marakwet. Pale kijijini alikozikwa alijulikana sana kwa jina 'Chemu'

•Rekodi za shule ya msingi aliyosomea Caroline zinaashiria kuwa alikuwa mwanafunzi mwenye nidhamu na alihudumu kama kinara.

Caroline Kangogo azikwa

Hatimaye afisa mtoro Caroline Kangogo anayedaiwa kujitoa uhai kwa kujipiga risasi kichwani amezikwa nyumbani kwa wazazi wake  katika kijiji cha Nyawa, kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Mamia ya waombolezaji ikiwemo maafisa wa polisi zaidi ya 20 kutoka kituo cha polisi cha Nakuru alikokuwa anahudumu Bi Caroline walihudhuria hafla ya mazishi. 

Hata hivyo, saluti 21 za bunduki hazikuwepo kama ilivyo desturi katika mazishi ya polisi yeyote  aliyeaga nchini.

Mwili wa Caroline ulivalishwa gauni la harusi kama alivyokuwa ameomba kupitia ujumbe wa simu.

Marehemu pia alikuwa ameomba asizikwe nyumbani kwa aliyekuwa mumewe ila azikwe kwa wazazi wake Elgeyo Marakwet. Pale kijijini alikozikwa alijulikana sana kwa jina 'Chemu'

Rekodi za shule ya msingi aliyosomea Caroline zinaashiria kuwa alikuwa mwanafunzi mwenye nidhamu na alihudumu kama kinara.

Wanafamilia wengi hawakuamini kuwa 'Chemu' waliyejua ndiye alitekeleza mauaji ya wanaume wawili mapema mwezi huu.

Kakake marehemu, Mark Kangogo alisema kuwa dadake  alikuwa mtu mzuri licha ya yale yaliandikwa kumhusu kwenye vyombo vya habari.

"Kama alitekeleza mauji yale kama ilivyoripotiwa basi ni vibaya. Hata niliuliza maafisa wakuu waliokuwa wanahudumu naye na walisema kuwa Caroline alikuwa afisa mzuri" Mark alisema.

Baadhi ya wanafamilia  walidai kuwa  hawakuwa wameridhishwa na  upelelezi uliokuwa unaendelea  na pia matokeo ya upasuaji wa mwili uliofanywa na mwapatholojia wa serikali Johansen Oduor.

Oduor alifanya upasuaji wa mwili wa Caroline  mapema wiki hii ni kudai kuwa risasi ilimwingia marehemu kwenye upande wa kulia wa kichwa na kutokea upande wa kushoto.

Hata hivyo alidai kuwa uchunguzi zaidi ungefanywa kubaini kama kwamba alijipiga risasi mwenyewe ama alipigwa na mtu mwingine.

Kifo cha Caroline kiliibua mdahalo mkubwa nchini huku maswali yakiulizwa ikiwa alijitoa uhai ama aliuliwa na mwili wake kubebwa hadi bafuni alikopatikana ionekane kama kwamba alijitoa uhai mwenyewe.

Kunao baadhi ya wataalam waliotilia shaka ikawaje marehemu akajipiga risasi na kubaki na bastola aliyotumia mkononi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved