Mwanahabari Lulu Hassan na mumewe Rashid Abdalaa kupita kwenye ukuasa wao wa instagram walimtakia mtoto wao heri njema ya siku yake ya kuzaliwa.
Ndoa ya wanahabari hao ni ya kupigiwa mfano na wengi na kutamanika na wengi, wawali hao wamekuwa wakifanya kazi ya utangazaji pamoja kwa zaidi ya miaka 3.
Lulu Hassan alimuomba Mungu ampe mwanawe marafiki wa kweli na kumzunguka na amani.
Ni matamanio ya kila mzazi kumuona mwanawe anakuwa na akiwa na afya njema kila kuchao.
"Nimemjua huyu champ kwa miaka kumi sasa 😂😂😂❤️❤️❤️na na siku hii naomba kwamba Mwenyezi Mungu azunguke na amani, ustawi, marafiki wa kweli, furaha ya kweli siku zote za maisha yako mazuri na muhimu zaidi afya njema❤️❤️ ❤️
Karibu katika awamu ya tarakimu mbili ❤️❤️🙏🏽," Aliandika Lulu.
Mumewe naye alikuwa na haya ya kumwandika mwanawe akisherehekea siku yake ya kuzaliwa;
"#sisemikitu Siku kama ya leo alizaliwa mwanangu Jibran. Haitakuwa dhambi tukimtakia heri njema na kumuombea mema,"
Hizi hapa jumbe za mashabiki;
neemasulubu: Happy birthday Jibran😍😍
nyakundi_isaboke: Happy birthday jibran
bridgetshighadi: Happy birthday handsome.. ❤️❤️
kanze_dena: Happy birthday jibby!!!
shiru103: Happy birthday🎂🎂🎂🎉🎉🎺🎈