logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Mungu ponya maumivu yetu,'Msanii Bahati ataka haki kutendeka kwa ndugu,2, wa Embu

Ndugu hao wawili walizikwa Ijumaa tarehe 13 nyumbani kwao katika kaunti ya Embu.

image
na Radio Jambo

Habari16 August 2021 - 07:19

Muhtasari


  • Benson Njiru na Emmanuel Mutura ambao walikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu na miaka kumi na tisa mtawalia,Ndugu hao wawili walifariki chini ya ulinzi wa polisi
  • Wawili hao walikuwa kutoka Kaunti ya Embu eneo la"Kianjokoma"
  • Ndugu hao wawili walizikwa Ijumaa tarehe 13 nyumbani kwao katika kaunti ya Embu
Bahati

Benson Njiru na Emmanuel Mutura ambao walikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu na miaka kumi na tisa mtawalia,Ndugu hao wawili walifariki chini ya ulinzi wa polisi.

Wawili hao walikuwa kutoka Kaunti ya Embu eneo la"Kianjokoma".

Ndugu hao wawili walizikwa Ijumaa tarehe 13 nyumbani kwao katika kaunti ya Embu.

Ilikuwa ni siku ambayo ilikuwa imejaa huzuni haswa kwa mama wa wawili hao.

Wakenya,wasanii,wanamitandao waliandamana mitandaoni  ili haki itendeke kwa ajili ya ndugu hao wawili.

Sio mmoja au wawili,bali asilimia kubwa ya wakenya walikashifu mauaji hayo.

Msanii Bahati kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliomba haki itendeke, na kuomba Mungu aponye maumivu ya jamaa ya wawili hao.

"Mungu mpendwa; Nani atatuponya kutokana na maumivu haya ya moyo yasiyovumilika ??? πŸ’” Mama apoteza Wanawe wawili Vijana na wasio na hatia mikononi mwa wale Ambao Wanatakiwa Kutulinda na Mpaka Sasa Hakuna Mtu Ambaye Amefikishwa Kwenye Haki ??? 😭😭😭

Ninapoangalia Picha hii Nakosa Manukuu; Huu ni Uchungu mimi binafsi sijaweza kuhimili kuutazama kwenye Habari za Runinga😭😭😭 MPENDWA MUNGU; WAWEZA KUONA MACHOZI YETU YA MACHOZO NA KULIPA KISASI KWA MBELE YETU πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ™πŸ™πŸ™," Aliandika Bahati.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved