Huku macho yote yakiwa kwenye mahakama ya rufaa, ili kutoa uamuzi wa BBI, baadhi ya wandani wa kinara wa ODM Raila Odinga wameanza kumuomba Mungu asaidia mchakato wa BBI.
Mapema wiki hii kinara huyo akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba, mahakama ya rufaa ikitupilia mbali mchakato wa BBI, hawataharibu muda wa kuenda kwenye mahakama kuu.
Jopo la majaji saba wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na Jaji Daniel Musinga wanatarajiwa kutoa uamuzi ambao utakuwa na athari kubwa kwa mchakato wa marekebisho ya katiba.
Rufaa hiyo iliwasilishwa na miongoni mwao rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga waliopinga uamuzi wa mahakama kuu uliyoharamisha mchakato wa marekebisho ya katiba maarufu BBI.
Kupitia kwenye ukurasa wake mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino aliandika ujumbe huku akimuomba Mungu asaidia BBI.
"Mungu saidia BBI tafadhali," Babu Owino aliandika.
Hizi hapa jumbe za wanamitandao baada ya ujumbe wake Owino;
Ali Dayib: We're also praying to God so that BBI dies a natural death.
Omondi Brian: This thing is coming down very fast than a super sonic jet, today we must celebrate the end of impunity.
Robert Kimutai: Today you are very humble!!!
Ben O. Osuga: God has heard you. Reggae will continue.. Inshallah!
Vitalis Kipkosgei:Babu as you are singing,no body can stop raggae..we husters sing.nothing but prayers
Huku jaji Tuiyott aitoa uamuzi wake kuhusu BBI alipuuzilia mbali rufaa ya IEBC,pia jaji Sichale alisema kwamba IEBC haikukosea kuhakiki saini zilizokusanywa kwa ajili ya BBI.
