logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi 3 wa akiba kushtakiwa kwa mauaji

Kanda hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa za kiusalama ambazo zimesababisha miradi mingi kukwama.

image
na Radio Jambo

Habari27 August 2021 - 09:59

Muhtasari


•Washukiwa hao watatu walikamatwa Jumatano na kutambuliwa vyema na manusura wa risasi.

Polisi watatu wa akiba katika eneo la Elwak, Kaunti ya Mandera, wamekamatwa kwa kuhusiana na madai ya kuwapiga risasi wanaume wawil.

Wanaume hao wawili waliuawa kwa kupigwa risasi wakiwa ndani ya gari mnamo Juni 21. Nia ya mauaji haijathibitishwa, lakini maafisa hao wametambuliwa tayari.

Ali Abdi Ali, Mohamed Ibrahim Issack na Ahmed Mohamed Abdilatif wanashtakiwa kwa mauaji ya Kulow Adfan Hassan na Ahmed Abdi Garad, polisi walisema.

Hii inafuatia uchunguzi uliofanywa na DCI . ilipelekwa kwa Ofisi ya Mashtaka ya Umma, ambayo ilitoa idhini ya kushtakiwa.

Uchunguzi uligundua kuwa watatu hao wanadaiwa kupiga risasi kwa abiria wa Toyota Succeed walipokuwa wakisafirisha abiria kwenye barabara ya Elwak-Dololo wakielekea Wajir. Watu wawili waliuawa.

Dereva aliendesha gari hadi kituo cha polisi cha Elwak na kuripoti shambulio hilo.

Washukiwa hao watatu walikamatwa Jumatano na kutambuliwa vyema na manusura wa risasi.

Kanda hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa za kiusalama ambazo zimesababisha miradi mingi kukwama.

Changamoto hizo ni pamoja na mapigano kati ya koo, mashambulizi ya al Shabaab na ukosefu wa barabara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved