logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho:Mke wangu aliniambia ataenda Saudi Arabia kufanya kazi baada ya kukosana naye

KUlingana na Joseph amekuwa akifika nyumbani amechelewa, na kumfanya mkewe akasirike

image
na Radio Jambo

Habari03 September 2021 - 05:55

Muhtasari


  • KUlingana na Joseph amekuwa akifika nyumbani amechelewa, na kumfanya mkewe akasirike
  • Jamaa aeleza wasiwasi baada ya mkewe kudai ataenda Saudi Arabia

Katika kitengo cha patanisho bwana Joseph aliomba apatanishwe na mkewe ambaye walikosana mwezi jana.

KUlingana na Joseph amekuwa akifika nyumbani amechelewa, na kumfanya mkewe akasirike huku akimtishia kuenda saudi Arabia kufanya kazi.

"Naomba mnipatanishe na mke wangu. Kulingana na kazi yangu, ninarudi nikiwa nimechelewa akaona ni kama siko serious akaondoka na sasa ananiambia hawezi kurudi na anataka kwenda kufanya kazi Saudia

Mimi nimebadilika kabisa, nitakuwa nikirudi nyumbani saa mbili, sina mpango wa kando."

Huku mkewe Phoebian akizungumzia hali hiyo na sababu yao ya kukosana alikuwa na haya ya kusema;

""Nitajuaje umebadilika?... Shida yake anakuja nyumbani kama amechelewa na nikimuuliza anakuwa mkali. Sijawahi kumshuku kuwa na mpango wa kando. Ni vigumu kurejea sasa hivi, anipe muda nifikirie. Haniheshimu kama mkewe."

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved