logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Corona:Visa vya maambukizi ya corona vimefika 241,134 baada ya watu 704 kupatikana na corona

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,874,858.

image
na Radio Jambo

Habari07 September 2021 - 13:20

Muhtasari


  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 667 ni wakenya ilhali 37 ni raia wa kigeni,337 ni wanaume huku 367 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 241,134 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 10.4%

Watu 704 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,776 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 667 ni wakenya ilhali 37 ni raia wa kigeni,337 ni wanaume huku 367 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 241,134 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 10.4%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,421,663.

Mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka 1, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 104.

Hata hivyo watu 5 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,800 ya walioaga dunia.

Aidha watu 756 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 229,762, 689 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 67 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,815 ambao wamelazwa hospitalini, 4,053 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 147  katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,874,858.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved