logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtoto wangu mmoja ni wa ex wangu, lakini mume wangu anajua ni wake-Mwanamke atoboa siri

KUlingana na mwanamke huyo mume wake alikuwa anataka mtoto msichana

image
na Radio Jambo

Habari13 September 2021 - 14:55

Muhtasari


  • Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama,katikakitengo cha toboa siri, mwanamke mmoja alitoboa siri jinsi alimdanganya mtoto wa ex wake ni wake

Kuku wakiwa wengi huwa wanamwaya mtama,katikakitengo cha toboa siri, mwanamke mmoja alitoboa siri jinsi alimdanganya mtoto wa ex wake ni wake.

KUlingana na mwanamke huyo mume wake alikuwa anataka mtoto msichana, kwani aliachana na bibi wake wa kwanza kwa kumzalia watoto wavulana.

Hii hapa siri yake;

"Ulikuwa mwaka wa 2017 ambapo nilifanya ngono na ex wangu, na nikapata ujauzito ambapo niliambia mume wangu kwamba ujauzito huo ni wake

Huo wakati mume wangu hakuwa anataka watoto, kwani alikuwa amekosana na aliyekuwa bibi yake kwa kumzalia watoto wavulana pekeyake bali alikuwa anataka mtoto msichana

Haja yangu ilikuwa tu nipate mtoto, lakini Mungu akanibariki nikapata mtoto wa msichana, hadi leo mume wangu hajui kwamba kifungua mimba wangu sio wake lakini ni wa ex wangu

Nilikuwa naonana na ex wangu bado nikiwa kwa mume wngu, kwa sababu nilikuwa nampenda sana, nataka kumtobolea mume wangu siri kwamba kifungua mimba wetu sio wake lakini ni wa ex," Alisimulia.

Je una hakika kwamba watoto wote na mkeo ni wako au kuna vile alicheza?

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved