logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mlinicheka nilipokuwa sina kitu,'Willy Paul akana madai kwamba ni mchoyo

Kulingana na Willy Paul alisema kwamba baadhi ya wasanii enzi hizo walikuwa wanamcheka

image
na Radio Jambo

Habari02 October 2021 - 11:48

Muhtasari


  • Pia kuna baadhi ambao wamesalia kwenye tasnia ya nyimbo za injili wamekuwa wakidai kwamba wenzao hawawashiki mkono katika kazi yao ya usanii

Tasnia ya nyimbo za burudani imejawa na wasanii tofauti nchini, huku baadhi yao wakigura tasnia hiyo.

Tumewaona baadhi ya wasanii wakipigana vita vya maneno mitandaoni na wenzao bila ya kujali kuwa wanapaswa kuwaonyesha mashabiki wao mfano mwema.

Pia kuna baadhi ambao wamesalia kwenye tasnia ya nyimbo za injili wamekuwa wakidai kwamba wenzao hawawashiki mkono katika kazi yao ya usanii.

Msanii Mr Seed alimshambulia Willy Paul na kusema kwamba hawashiki wasanii wenzake mkono, ilhali alikuwa anaoma msaada kabla ya kupata umaarufu mkubwa.

Kulingana na Willy Paul alisema kwamba baadhi ya wasanii enzi hizo walikuwa wanamcheka kwani hakuwa na pea.

Paul aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram baada ya kupakia kibao ccha Mr Seed na msanii Masauti.

"seed my brother kumbuka mema ya mtu kabla mabaya. Wewe ni ndugu yangu ulisema sijawai kusaidia anyone..

kumbuka I came to ur event pale huruma free na sio hio tu. Ata kwa ruracio yako nika changa and I was even present

Remember zile siku I was a nobody na wewe na wasani wame make it mlikua mnani chekelea and making fun of me??..

Sai that God has made a way for me ndio wewe na wenzako mnaona ubaya wangu? Hii chuki yote ninya nini? Is there something ur not telling me?

Ndio song nime share tena. Keep up the good work but tukue tu na heart poa coz hatujui ya kesho. โœŒBug up @officialmasauti_ kwa kuongeza uzito kwa hii song ๐Ÿ‘ ๐Ÿ‘ ๐Ÿ‘,"Aliandika Willy Paul.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved