logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Niliahidi kuwajibika!" Eric Omondi adai kwamba alimpachika mwanamuziki Miss P ujauzito

Omondi amedai kwamba walipatana na Miss P miezi mitano iliyopita katika tamasha ambayo alikuwa anafanya na baada ya hapo tamasha wakaamua kushiriki mchezo wa kitandani pamoja.

image
na Radio Jambo

Habari01 November 2021 - 08:28

Muhtasari


•Omondi amedai kwamba walipatana na Miss P miezi mitano iliyopita katika tamasha ambayo alikuwa anafanya na baada ya hapo tamasha wakaamua kushiriki mchezo wa kitandani pamoja.

•Mcheshi huyo amesema kuwa tayari amemhakikishia Miss P kuwa atawajibikia mtoto aliyebeba huku akidai kuwa watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.

•Haya yanajiri takriban wiki moja tu baada ya Omondi kuapa kuoa mshindi wa Wife Material, Monica Ayen na kupata watoto wengi warembo naye.

Mcheshi mashuhuri nchini Eric Omondi amejipata kuwa gumzo la mjini tena baada ya kudai kuwa anatarajia mtoto pamoja na mwanamuziki Miss P.

Kwenye mtandao wa Instagram wasanii hao wawili wamepakia picha inayomuonyesha Miss P akiwa mjamzito huku Omondi akiwa amemshika tumboni.

Akizungumzia picha hiyo, Omondi amedai kwamba walipatana na Miss P miezi mitano iliyopita katika tamasha ambayo alikuwa anafanya na baada ya hapo tamasha wakaamua kushiriki mchezo wa kitandani pamoja.

Mcheshi huyo amesema kuwa tayari amemhakikishia Miss P kuwa atawajibikia mtoto aliyebeba huku akidai kuwa watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.

"Nilipatana na mwanamke huyu mrembo miezi tano iliyopita  katika tamasha ambayo nilikuwa nafanya. Kilichotendeka kilitendeka na nilimuahidi kuwa nitawajibika. Watoto ni baraka kutoka kwa Mungu" Omondi aliadika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wanamitandao wengi ikiwemo watu mashuhuri wamejitokeza kuwapongeza wawili hao huku wengine wakidai kuwaujauzito ule si wa kweli ila ni kiki tu wanatafuta.

TeteSI imeibuka kwamba Miss P anapanga kutoa ngoma hivi karibuni na ndiposa akaamua kutumia madai ya ujauzito kutafuta kiki. 

Eric Omondi si mgeni kwa drama na anajulikana kuwa mbunifu sana katika utafutaji wa kiki.

Haya yanajiri takriban wiki moja tu baada ya Omondi kuapa kuoa mshindi wa Wife Material, Monica Ayen na kupata watoto wengi warembo naye.

"Monica Ayen-Omondi. Hongera kwa kushinda moyo wangu. Hongera kwa kushinda shoo ya mwisho ya Wife Material. Naahidi kukupatia mapenzi yangu yote. Nitakuheshimu. Nitakuheshimu kwa utu wangu wote. Naahidi kukulinda. Siwezi kusubiri kuanzisha familia pamoja nawe. Siwezi subiri kupata watoto warembo na wewe. Wewe sio tu mwanamitindo bali una moyo mzuri. Unanikamilisha kipenzi. Unanikamilisha mpenzi wangu" Eric alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved