logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sijaamini,nina kilio moyoni,'Mama wa kijana aliyeuawa katika shule ya wasichana azungumza

Pia alisema kwamba aliambiwa kesi hiyo iko kwa DCI, ili kubainisha nini kilichosababisha kifo cha mwanawe.

image
na Radio Jambo

Habari01 November 2021 - 08:30

Muhtasari


  • Mama wa kijana aliyeuawa katika shule ya wasichana azungumza

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Mary Mbage, mama ya mwanafunzi aliyeaga dunia kutokana na majeraha ya kupigwa alipopatikana akinyemelea bweni la wasichana Kiambu.

Kulingana na Mary amekuwa akiwalea wanawe pekeyake, lakini kinachosikitisha ni kuwa hajui hasa mwanawe alichapwa au kupigwa na nini ili apoteze maisha yake.

Pia alisema kwamba aliambiwa kesi hiyo iko kwa DCI, ili kubainisha nini kilichosababisha kifo cha mwanawe.

"Tulimzika lakini, hajatoka moyoni mwangu, nina muona kila siku, kwa nyumba hamna amani ni kilio tu

Kwani ndugu yake ambaye yuko darasa la tano anashinda kusema kwamba anamtaka ndugu yake,ninaumia moyoni nataka haki itendeke kwa mwanangu

Siwezi sema mtoto wangu aliuawa na nani au na nini na wala aliaga dunia akiwa hospitali au akiwa shuleni," Alieleza Mary.

Mary aliendelea na kusema kwamba hawezi mtoa mwanawe moyoni kama vile amekuwa akiambiwa na watu.

"Baada ya mazishi sasa ndio naona ukweli kwamba mtoto wangu hayupo, nimepata ushauri na kuambiwa kwamba napaswa kumtoa moyoni, lakini siwezi kama mama nimekuwa naye tangu alipozaliwa

Sisemi kwamba mwanangu alifanya kitu kizuri kuenda kwenye shule ya wasichana, lakini wale walimuua hawakufanya jambo nzuri, wangempeleka polisi

Hatukupeleka watoto wetu shuleni warudi  kwenye majeneza."

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved