logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanafunzi wanne watiwa mbaroni kwa kupanga kuteketeza bweni Murang'a

Wanne hao walikamatwa siku ya Jumatatu baada ya camera za CCTV kumulika  mmoja wao akirusha barua kwa ofisi ya mwalimu mkuu, Mutero Ndiiwa iliyomwagiza awaruhusu waende nyumbani kabla ya Ijumaa na kutishia kuchoma bweni iwapo angekosa kuwapa ruhusa.

image
na Radio Jambo

Habari09 November 2021 - 02:56

Muhtasari


•Wanne hao walikamatwa siku ya Jumatatu baada ya camera za CCTV kumulika  mmoja wao akirusha barua kwa ofisi ya mwalimu mkuu, Mutero Ndiiwa iliyomwagiza awaruhusu waende nyumbani kabla ya Ijumaa na kutishia kuchoma bweni iwapo angekosa kuwapa ruhusa.

•Siku ya Jumapili mwalimu mkuu  alipokea simu kutoka kwa naibu wake Jane Wamunya akimfahamisha kuwa mlinzi alikuwa amepata lita tano za petroli zilizkuwa zimefichwa kwenye uzio wa shule.

Polisi katika kituo cha Githumu, kaunti ya Murang'a wanazuilia wanafunzi wanne kutoka shule ya upili ya Gituro ambao wanaripotiwa kushirikiana kupanga njama ya kuteketeza bweni.

Wanne hao walikamatwa siku ya Jumatatu baada ya camera za CCTV kumulika  mmoja wao akirusha barua kwa ofisi ya mwalimu mkuu, Mutero Ndiiwa iliyomwagiza awaruhusu waende nyumbani kabla ya Ijumaa na kutishia kuchoma bweni iwapo angekosa kuwapa ruhusa.

Bwana Mutero aliripoti kwamba mnamo siku ya Jumapili alipokea simu kutoka kwa naibu wake Jane Wamunya akimfahamisha kuwa mlinzi alikuwa amepata lita tano za petroli zilizkuwa zimefichwa kwenye uzio wa shule.

Kulingana na taarifa ya polisi iliyoandikwa na mwalimu mkuu, mafuta yale yalikuwa yamepangwa kutumiwa kuteketeza bweni moja katika shule hiyo.

Wanafunzi wanne ambao walikamatwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani  leo (Jumanne) ili kujibu mashtaka dhidi yao.

Haya yanajiri huku visa vya uchomaji wa shule vikiwa vimekithiri 

Siku ya Jumatatu wanafunzi watatu kutoka shule ya Kagumo, kaunti ya Nyeri walikamatwa walipokuwa wanajaribu kuteketeza bweni moja katika shule hiyo. Watatu hao walipatikana na petroli, tapentaini pamoja na kiberiti.

Takriban shule tano ziliripoti visa vya moto usiku wa kuamkia Jumatatu.

Shule hizo ni pamoja na Mwala Girls High katika Kaunti ya Machakos, Maranda High katika Kaunti ya Siaya, Cheplaskei High iliyoko Uasin Gishu, Shule ya Upili ya Wavulana ya Nambale iliyoko Busia na Shule ya Msingi ya St. Mary's Riabore katika Kaunti ya Nyamira.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved