logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Taliban yapiga marufuku wanawake kushiriki vipindi vya kuigiza katika runinga

Waandishi wa kike na watangazaji pia wametakiwa kuvalia hijabu katika runinga

image
na Radio Jambo

Habari22 November 2021 - 06:32

Wanawake wamepigwa marufuku kushiriki katika vipindi vya runinga nchini Afghanistan katika sheria mpya iliowekwa na serikali ya Taliban.

Waandishi wa kike na watangazaji pia wametakiwa kuvalia hijabu katika runinga , ijapokuwa maelezo hayo mapya hayasemi wanafaa kujifunika kwa namna gani.

Waandishi wa habari wanasema baadhi ya sheria hazieleweki na zinapaswa kutafsiriwa.

Taliban lilichukua madaraka nchini Afghnistan katikati ya mwezi Agosti na wengi wanaohofia wanaweka sheri kali.

Kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu, ambalo lilichukua udhibti wa taifa hilo kufuatia kuondoka kwa vikosi vya Marekani na washirika wake pia viliwataka wasichana na wanawake kutoenda shule.

Wakati wa utawala wao miaka ya tisini , wanawake walipigwa marufuku kupata elimu na kufanyakazi.

Maelezo ya hivi karibuni ya Taliban , ambayo yametolewa na runinga ya Afghanistan yalishirikisha sharia nane.

Kupiga maraufuku filamu zinazofikiriwa kwenda kinyume na sheria ya Kiislamu huku picha za wanaume wanaonesha miili yao pia ikipigwa marufuku. Vipindi vya kuchekesha na vya burudani vinavyotusi dini ama ambavyo vinaweza kuonekana kwenda kinyume na mafunzo ya dini pia havitakiwi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved