logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilikuwa nimekonda sana-King Kaka afichua sababu ya kubadilisha picha ya EP yake

Alisema picha ya awali alikuwa amekonda na mgonjwa haikuweza kuendana na jalada la EP

image
na Radio Jambo

Habari01 December 2021 - 08:58

Muhtasari


  • King Kaka afichua kwa nini alibadilisha picha ya EP yake

Rapa King Kaka alisherehekea EP yake ya kwanza katika kipindi cha miaka 13 inayoitwa 'Happy hour' jana usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwanamuziki huyo  alitoa maelezo machache kuhusu utengenezaji wa EP yake, afya yake na kile ambacho amekuwa akikifanya.

Kaka alieleza kwa nini alibadilisha picha ya jalada lake, akitumia picha ya mkewe Nana badala yake.

Alisema picha ya awali alikuwa amekonda na mgonjwa haikuweza kuendana na jalada la EP hivyo akaamua kubadilika.

"Tulipiga picha kwenye jalada lakini nilikuwa nimekonda sana na nilikuwa mgonjwa kwa hiyo, haikufanya kazi. Tuliamua kumpigia simu mke wangu kwa kuwa amekuwa na jukumu muhimu katika maisha yangu

Leo ni ya kusherehekea maisha yangu. Hapo awali, sikujua jina lilimaanisha nini lakini sasa hivi, najua kila siku ni saa ya furaha. Nataka kuthamini maisha zaidi na ninataka kusaidia watu zaidi."

Kaka alisema awali EP yake ilitakiwa kutolewa Oktoba lakini alipougua, walibadilisha tarehe.

Akizungumzia afya yake, Kaka alisema ameimarika.

"Mimi ni mzima wa afya, siamini. Nilikuwa na kilo 85 na kufikia kilo 62. Ilikuwa ni kichaa sikuwa natembea, naweza kula na sikuwa na maumivu, nilipungua tu."

Alieleza sababu iliyomfanya hataki kuzungumzia afya yake na mashabiki wake ni kwamba alitaka kupigana vita na marafiki zake wa karibu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved