Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini Tanzania kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Mkuu wa Nchi ya Tanzania Samia Suluhu.
Rais aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi na baadaye kuhudhuria sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa nchi hiyo.
Sherehe hiyo ilifanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Rais Kenyatta ambapo alikuwa mgeni mkuu.
Rais Kenyatta ni miongoni mwa Wakuu wa Nchi na Serikali walioalikwa na Mheshimiwa Samia Suluhu kuhudhuria Sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Tanzania.
His Excellency President Uhuru Kenyatta arrives in Dar es Salaam, Tanzania for a two-day State Visit during which he was the Chief Guest at celebrations to mark the 60th anniversary of Mainland Tanzania's independence. @ForeignOfficeKE | @SuluhuSamia pic.twitter.com/kxwdQRXm8I
— State House Kenya (@StateHouseKenya) December 9, 2021
