Katika kitengo cha patanisho Bi Stella,25 alituma ujumbe ili apatanishwe na mumewe Joseph 53,ambaye wamekuwa pamoja kwa mwaka mmoja sasa.
Kulingana na Stella anamtaka mumewe amjengee nyumba ili aweze kubeba ujauzito wake.
"Nataka nipatanishwe na mume wangu, hatujaachana lakini hatujakuwa tukielewana kwa muda sasa,alinioa baada ya mke wake kuaga dunia mwaka jana
Kuna mtoto wake ambaye haniheshimu, nampenda mume wangu, lakini nataka anjengee nyumba ili nimzalie na mimekuwa nikimwambia hivyo lakini haskii
Sitaki watoto wangu wateseke nataka nyumba yangu ambayo watoto wangu watasema ni ya mama yao
Pia awache kunilazimisha kufanya tendo la ndoa," Alieleza Stella
Baada ya kufanya juhudi za kumtafuta Joseph alikuwa na haya ya kusema kuhusu matamshi yake Stella.
"Nitafanya kila kitu ambacho anataka, pia nitawaaabia watoto wangu wamheshimu mama yao, kwa maana ninampenda, pia nitamjengea."
Kwa uhondo zaidi tembelea Radio jambo Youtube.