Mbunge wa Kandunyi Wafula Wamunyinyi amesema uzinduzi wa chama chake kipya cha DAP-K siku ya Jumanne ulikuwa muhimu kwa kulinda jamii ya magharibi dhidi ya kutumiwa vibaya na wanasiasa wanaotaka kura zao.
Chama hicho kilizinduliwa katika ukumbi wa Bomas of Kenya baada ya mrengo wa Ford Kenya ambao unaongozwa na Moses Masika Wetang’ula kukataa kuafikiana na waasi hao.
Mbunge huyo pamoja na mwenzake wa Tongaren Eseli Simiyu waliungana na kuunda chama cha DAP-K wakikusudia kukitumia kuleta pamoja watu wa magharibi.
Akiwa kwenye mahojiano katika kituocha Citizen, Wamunyinyi alisema vyama vingine vimekuwa vikiwanyanyasa watu wa Magharibi na wametosheka na hulka yao
“Chama kidogo kinachoongozwa na Musalia kimetumika kuwanyanyasa watu wa Magharibi na tumetosheka.Ni lazima waelewe; na wajue kuwa tunaenda mashinani kuhakikisha haturuhusu watu wetu kutumiwa tena,” Wamunyinyi alisema
Aliendelea kusema chama cha Dap-k ni cha kidemokrasia ambacho kinasimamia umoja wa nchi na wangependa kuona jamii yenye usawa.
Kuunda chama kipya nchini sio jambo geni kwanivyama vingi vimevujwa huku vingine vipwa vikizaliwa
Wamunyinyi alitaja mzozo kati yake na Wetangula kama sababu kuu ya kugura chama cha Ford Kenya na kuunda kingine.
Walipohojiwa ni kwa nini chama kilichagua kutosimamisha mgombeaji urais mwaka ujao ili kuidhinisha kampeni ya Azimio la Umoja ya Raila Odinga, chama hicho kilisisitiza kuwa DAP-K ni chama changa ambacho hakina nia ya kuwasilisha ombi la urais kwa haki. kwa ajili yake.